Magaidi wa Daesh, leo wamefanya mashambulizi makali katika ofisi na majengo ya serikali katika mji wa Ramadi nchini Iraq, kama sehemu ya azma yao ya kuuteka kikamilifu mji huo wa magharibi mwa Baghdad. Magaidi hao waliokuwa na silaha nzito walifyatua risasi wakiwa katika mapaa ya majengo ya ofisi za serikali na makao makuu ya polisi huku askari na wapiganaji wa kikabila wakijaribu kukabiliana na magaidi hao ili wasiweze kuusogelea zaidi mji huo. Matangazo misikitini yametoa wito kwa wapiganaji zaidi kujitokeza kupambana na magaidi hao wasiona huruma wasiweze kuuteka mji wa Ramadi, ambao kama utachukuliwa litakuwa pigo kubwa kwa majeshi ya serikali ambayo yalivunja udhibiti wa magaidi hao katika kiwanda kikubwa zaidi cha usafishaji mafuta katika eneo hilo mapema wiki hii. Sehemu kubwa ya mji huo na jimbo la Anbar kwa jumla liko mikononi mwa magaidi hao.
Yafaa kuashiria kwamba magaidi hao wamekuwa wakiuza mafuta kupitia uturuki, magaidi hawa pia wanatuhuma za ubakaji, uuaji na kuuza wanawake mateka.